Waziri Mkuu: Sukari Haitakuwa Tatizo Ramadhani
WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja
isizidi Sh 2,300.
Alisema
hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi
wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha
Mipango mjini hapa.
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani
nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada
kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.
Pia
alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na
nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000
zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.
Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.
“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema.
“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”
Alisema
suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na
Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia
sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.
Alitoa
mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji
ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo.
Katika
miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini,
imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh
takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka
wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka
nje ili kukabili upungufu uliopo.
No comments