Juma Nkamia Adai Wapinzani Wanasura Mbaya Kiasi Kwamba Wanataka Kutapika na Wengine Meno Yao Yameoza!
Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo.
Jana
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliporomosha lugha za kuudhi baada
ya kuwaambia wabunge wa upinzani waliokuwa wakishangilia kuwa wanasura
mbaya hadi wanatamani kutapika.
Akichangia
hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi kwa mwaka 2016/17, Nkamia alionyesha kukerwa na hotuba ya
upinzani kuhusu wizara hiyo kwenye sehemu iliyozungumzia uchaguzi mkuu
wa Oktoba mwaka jana.
Nkamia
alisema uchaguzi umepita na mshindi alipatikana ambaye ni CCM na
aliufananisha uchaguzi na mpira kwamba unapoisha uwanjani mtu hawezi
kulalamika nje.
“Uchaguzi umeisha, leo mtu anasimama hapa anasema ‘ooh tuliibiwa kura’ mlikuwa wapi wakati mnaibiwa kura?”alihoji na kuwataka wapinzani watafute sababu kwa nini walishindwa na si vinginevyo.
"Wanajua
mchezaji mmoja akiumia katika timu unachukua mwingine kwenye timu ile
ile lakini inakuwaje unachukua mchezaji kutoka upinzani? Kwa hiyo
niwaombe tu muwe mnatafakari kwanza,” alisema.
Hali
hiyo iliibua kelele na minong’ono kutoka kwa wapinzani, jambo ambalo
lilimlazimu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka wabunge huku akiwataja
majina watulie ili mbunge huyo amalizie mchango wake.
Nkamia aliendelea, “We
nyosha midomo, fanya nini lakini that is the truth (huo ndiyo ukweli).
Utaongea sana na utapiga kelele sana lakini ukweli ndio huo na
umekuingia vizuri.
"Mimi
kelele wala hazinisumbui. Mimi nataka niwashauri kama wakati ujao
mnataka kuwa chama kizuri anzeni kutafuta wachezaji wenu,” alisema.
“Nyie pigeni kelele lakini ukweli ndio huo, wenye akili wanajua na wapiga kelele wanajua na najua limewaingia vizuri sana.”
Kijembe
hiki kiliwalenga Ukawa ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walimteua
aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa. Ukawa walimteua Lowasa baada ya
kuitema na kuihama CCM ambapo alipambana na John Magufuli (CCM) aliyeshinda.
Nkamia akionekana kumlenga mbunge fulani ambaye hakumtaja jina alisema, “We piga kelele, kwanza meno yako yameoza.”
Kwa
kuzingatia kanuni, lugha hiyo ni ya kuudhi lakini Dk Tulia asisitiza
Nkamia amalizie kuchangia ambapo alitoa mfano wa mwandishi wa vitabu
Bernard Taper aliyewahi kusema kwamba kuna watu wakiamka asubuhi
wakijiangalia kwenye kioo wanatamani kutapika.
“Sasa nyie mnaoshangilia humu mna sura mbaya na mnatamani kutapika,” alisema Nkamia
No comments