#UCLFinal: C. Ronaldo – Rekodi 2 anazoweza kuzivunja, ataweza kuondoa ukame wa San Siro, na vitu wanavyotakiwa kufanya Atletico kumzuia asiwadhuru
Cristiano Ronaldo alifunga mara ya mwisho Real Madrid walipokutana na Atletico katika fainali ya UEFA Champions League, lakini je atafanikiwa kuwafunga tena? Tuangalie takwimu muhimu kuhusu Cristiabo Ronaldo kuelekea mchezo huu.
1. Rekodi za kuvunja
Ikiwa kuna rekodi za kuvunja basi Cristiabo Ronaldo atajaribu kuzivunja; kwenye fainali ya Jumamosi kuna kuna rekodi kubwa tatu za kuvunja. CR7 ameshafunga magoli 16 katika mashindano haya msimu huu na anahitaji goli lingine ili kuifikia rekodi yake ya kufunga magoli mengi zaidi katika msimu mmoja wa UCL – rekodi aliyoiweka msimu wa 2013/14. Pia anaweza kuifikia rekofi ya Lionel Messi kuwa mfungaji bora katika misimu minne mfululizo.
Anaweza pia kumzidi Messi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali 3 za Champions League. Ronaldo ni mmoja ya wachezaji 16 ambao wameshafunga katika fainali mbili za ulaya, lakini pia ana safari ndefu ya kuifikia rekodi ya Alfredo di Stefano ya kufunga magoli katika mechi 5 za fainali za ulaya (1956, 1957, 1958, 1959, 1960)
Kufunga goli ndani ya San Siro – Milan
Stadio San Siro ni uwanja mgumu kwa Ronaldo, hajawahi kufunga goli katika uwanja huo. Ameshacheza dakika 360 za UEFA Champions League kwenye uwanja huu – mechi 3 na Manchester United na moja na Real Madrid – lakini hajawahi kufunga goli – au kuwa katika kikosi kilichoshinda katika uwanja huu.
Rekodi za Cristiano Ronaldo katika uwanja wa San Siro (W0 D2 L2)
AC Milan 2-2 Real Madrid, 03/11/10
Internazionale 0-0 United, 24/02/09
AC Milan 3-0 United, 02/05/07
AC Milan 1-0 United, 08/03/05
Kufunga vs Atletico
Nahodha huyo wa Ureno ameshaifunga Atletico Madrid magoli 15 katika mechi 24 – katika michuano ya La Liga, Copa, Spanish Super Cup – hat trick moja katika ushindi wa 4-1 ugenini mnamo April 2012, ameshawahi kupewa kadi nyekundu katika fainali waliyofungwa 2-1 ya Copa del Rey.
Kwa ujumla amecheza dakika 2,117 dhidi ya Atletico, ana wastani wa kuwafunga katika kila dakika 141. Japokuwa kwa sasa ana ukame wa kutokuwafunga katika 487 – mara ya mwisho kuwafunga ilikuwa kwenye mchezo wa Copa del Rey waliotoka sare ya 2-2 mnamo January 2015.
Vitu wanavyotakiwa kufanya Atlético ili asiwadhuru.
1) Kujihadhari na penati; magoli 7 kati ya 15 aliyowafunga Ronaldo yalitokana na mikwaju ya penati.
2) Kumpa udhibiti maalum katika dakika 25 za mwanzo za mchezo; takwimu zinaonyesha katika magoli 15 aliyowafunga – 8 aliyafunga ndani ya dakika 25 za mwanzo na manne kati ya hayo ni katika dakika ya 22 mpaka ya 25.
Takwimunza Cdistiano Ronaldo vs Atletico katika mechi zote.(W12 D5 L7)
90: Madrid 3-2 Atlético, 28/03/10
90: Madrid 2-0 Atlético, 07/11/10
90: Madrid 3-1 Atlético, 13/01/11 (Copa del Rey) – one goal: 60
90: Atlético 0-1 Madrid, 20/01/11 (Copa del Rey) – one goal: 22
70: Atlético 1-2 Madrid, 19/03/11
90: Madrid 4-1 Atlético, 26/11/11 – two goals: 23pen, 82pen
90: Atlético 1-4 Madrid, 11/04/12 – three goals: 24, 67, 82pen
90: Madrid 2-0 Atlético, 01/12/12 – one goal: 15
115: Madrid 1-2 Atlético, 17/05/12 (Copa del Rey) – one goal: 14, shown red card in extra-time
90: Madrid 0-1 Atlético, 28/09/13
90: Madrid 3-0 Atlético, 05/02/14 (Copa del Rey)
74: Atlético 0-2 Madrid, 11/02/14 (Copa del Rey) – two goals: 6pen, 15pen
90: Atlético 2-2 Madrid, 02/03.14 – one goal: 81
120: Madrid 4-1 Atlético, 24/05/14 (UEFA Champions League final) – one goal: 120pen
44: Madrid 1-1 Atlético, 19/08/14 (Spanish Super Cup)
45: Atlético 1-0 Madrid, 22/08/14 (Spanish Super Cup)
90: Madrid 1-2 Atlético, 13/09/14 – one goal: 25pen
28: Atlético 2-0 Madrid, 07/01/15 (Copa del Rey)
90: Madrid 2-2 Atlético, 15/01/15 (Copa del Rey) – one goal: 53
90: Atlético 4-0 Madrid, 07/02/15
90: Atlético 0-0 Madrid, 14/04/15 (UEFA Champions League quarter-final)
90: Madrid 1-0 Atlético, 22/04/15 (UEFA Champions League quarter-final)
90: Atlético 1-1 Madrid, 04/10/15
90: Madrid 0-1 Atlético, 27/02/16
No comments