Header Ads

Mourinho: Mambo 10 ya kufanya kuelekea kwenye mafanikio Man Utd – Part 2


Hatimaye Louis van Gaal amesitishiwa mkataba wake na Manchester United na dakili zite zinaonyesha kwamba Jose Mourinho atamrithi Mdachi huyo.
Jose anakuja Man United akiwa anategemea kuinasua klabu hapa ilipokwama kuelekea kwenye mafaniko waliyozoea.
Katika kufanikisha haya yote – Mourinho ana mambo ambayo atayapitia kuelekea kwenye mafanikio na Man United – Tuanze kuyahesabu na kuyaelezea kwa awamu.
Sehemu ya pili
  7. Kuwavuta upande wake wote wenye mashaka juu yake.
Manchester United wana utamaduni wao na staili ya soka na Sir Bobby Charlton ameshaeleza huko nyuma mashaka yake juu ya Mourinho.
Pia kuliwahi kuwa na taarifa kwamba Ferguson hakuwa anaunga mkono wazo la Mourinho kupewa timu na inaonekana Man United watamwambia kocha huyo aondokane na tabia ya ukorofi ambayo imekuwa ikimletea matatizo kwenye maisha yake ya soka. Mourinho anajielewa sana na anatambua  kuwa kwamba wapo ambao wanamuona kwamba Hafai kushika nafasi hiyo – anaweza kuwatuliza wote wenye mashaka nae.
 6. Kuwapa Nafasi Vijana wachanga
Manchester United wana utajiri mkubwa kwa kuvikuza vipaji vya wachezaji wao wachanga mpaka kukua kwao na kujiunga na timu ya wakubwa. Hapo zamani kulikuwa na  “the Busby Babes” katika miaka ya 1950s na baada kikosi  “The Class Of 92” kikosi kilichokuwa na wachezaji kama Giggs, Paul Scholes, Gary na  Phil Neville, David Beckham pamoja na Nicky Butt.
Mourinho, kwa upande mwingine amepata sifa ya kutowaamini sana wachezaji wachanga – mfano ni wachezaji kama Romelu Lukaku na Kevin de Bruyne walishindwa kabisa kuwa bora chini ya Mourinho.
Iliwabidi kwenda sehemu nyingine na kuweza kufikia ubora wao. De Bruyne  aliuzwa kwenda Wolfsburg kwa £19m mnamo January 2014 wakati Lukaku aliuzwa kwenda Everton mnamo June 2014 kwa ada ya £28m deal. De Bruyne, 24, amehamia Manchester City kwa ada ya £55m dirisha lilopita la usajili na Lukaku alifunga magoli 18 akiwa na Everton msimu huu. Kwa sasa anauhusishwa na kujiunga na Chelsea kwa ada ya £65m.
Mourinho tayari atakuwa na vijana wa kufanya nao kazi akiwemo mmoja wa wachezaji wa United msimu huu Marcus Rashford na Anthony Martial, mfungaji wa goli la ushindi la kombe la FA Cup – Cameron Borthwick-Jackson na Timothy Fosu-Mensah wote walipewa nafasi na wameonyesha kile wanaweza kufanya.
.
5. Pata mafanikio kwa staili
Sifa ya Old Trafford ya  “Theatre Of Dreams” imeharibiwa na soka bovu la kipindi cha miaka mitatu chini ya Moyes na Van Gaal – na maswali yameshaanza juu ya Mourinho na mbinu anazotumiaga kushinda.
Atahitaji kurudisha utamaduni wa united pamoja kuunganisha na mchezo wake a hii itarudisha ile excitement ya United huku wakishinda kwa staili nzuri kama ilivyokuwa chini ya Sir Alex Ferguson.
  Wakati Chelsea waliposhinda ubingwa msimu wa 2015, walifunga magoli 73, magoli 10 pungufu ya yale waliyofunga Manchester City walioshika nafasi ya pili lakini magoli mawili zaidi ya Arsenal ambao husifiwa kucheza sokala kushambulia zaidi.
Alipochukua ubingwa wa EPL msimu wa 2005-06, walifunga magoli sawa na United walioshika nafasi ya pili – magoli 72, lakini wao hawakufungwa magoli mengi  – magoli 22 na United waliruhusu 34.
  Wakati aliposhinda La Liga na Madrid msimu wa  2011-12, rekodi zake zilikuwa bora sana – walifunga magoli mengi zaidi kwenye historia ya ligi – magoli 121, walikuwa utofauti wa magoli  +89, na walipata pointi nyingi zaidi- 100. 

No comments

Powered by Blogger.