Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki
zilizokuwa zikitumika kuweka mishahara ya watumishi hewa, kurejesha
fedha hizo serikalini ; au kubainisha waliokuwa wakitumia akaunti hizo,
kuchukua fedha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Makonda alisema benki ndio pekee wanaoweza
kusaidia mkoa, kutambua wahusika waliokuwa wanatumia akaunti hizo
pamoja na wale waliokuwa wanachukua fedha hizo.
Alisema
watu hao wasipopatikana, inamaanisha fedha bado zipo katika benki hizo,
hivyo zinapaswa kuzirudisha serikalini zifanye maendeleo kwa wananchi.
“Tayari
tumeshaziandikia benki hizo barua na kuwapatia majina na akaunti na
kuwataka kutuwasilishia majina ya wahusika, waliohusika na akaunti hizo
ili kusaidia kutambua mtandao mzima wa wahusika wa suala la watumishi
hewa ambao wameigharimu serikali,” alisema Makonda.
Alitaja
benki hizo pamoja na fedha wanazodai kuwa ni benki ya NMB ambayo
inadaiwa zaidi ya Sh bilioni mbili, CRDB zaidi ya milioni 400, NBC zaidi
ya milioni 141, DCB milioni 85, Standard Chartered zaidi ya Sh milioni
mbili na Community Benki zaidi ya milioni 100.
“Hakuna
mtu anayeweza kutumia akaunti ya mtu bila kufuata taratibu za kibenki,
hata kama mtu amefariki kuna taratibu za kufuata ndipo apate akaunti,
naamini benki hizi zitasaidia kuwatambua wahusika wote,” alisisitiza.
Aidha, alizitaka benki hizo kufunga huduma za akaunti hizo ;na zisifanye malipo yoyote mpaka fedha hizo zitakapopatikana.
Mpaka
sasa, Mkoa wa Dar es Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 283,
ambao wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 3.6 ambazo
zilitumika kuwalipa mishahara.
No comments