SAUTI, MKUU WA WILAYA CHUNYA BI,REHEMA MADUSA AZITAKA TAASISI ZILIZOPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA WACHIMBAJI KUWAJIBIKA
Mkuu wa wilaya ya chunya mkoani mbeya BI. REHEMA MADUSA amewataka wananchi
kuchukua taardhari mapema dhidi ya
majanga yanayoweza kuepukika katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.
Hayo yamejili baada ya watu watatu kupoteza maisha kwenye dimbwi la maji katika jiji cha mtumbo kata ya chalangwa wilayani humo walipokuwa wakisafisha madini ambapo walitumbukia na kukosa hewa ya oxygen.
Hata hivyo madusa amewataja marehemu kuwa
wawili ni wa familia moja ZAWARD
SODA [28] WILISON SODA[24] na JAML OMAL
[20] ambao walikuwa wakijishughurisha na shughuli za uchimbaji wa madini katika
kata hiyo.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa hali inatokana na jamii kukosa
elimu hivyo amewataka wakuu wa idara
kutoa elimu kwa jamii juu ya taadhari dhidi ya majanga mbali mbali
yanayoweza kuepukana.
Pia Mh, Madusa amewataka Osha na wasimamizi wengine ambao wamekuwa
wakichukua kodi kwa wachimbaji kuhakikisha wanasimamia mazingira na usalama wa
wachimbaji ,ili kuweza kuepusha baadhi ya majanga yanayoweza kutokea nchini hasa migodini.
No comments