MKUU WA MKOA WA MBEYA ATANGAZA VITA NA MAJAMBAZI AWAOMBA WANANCHI USHIRIKIANO
– Awataka Majambazi wautangaze Mkoa wa Mbeya si Mkoa salama Kwao
-Walioshindikana Tanga na Mwanza walikamatiwa Mbeya
– Alimwagia sifa jeshi la polisi na kulitaka kuongeza nguvu
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola hususani jeshi la polisi katika operesheni YA dhibiti ujambazi Mkoa wa Mbeya ili Mkoa huo uendelee kuwa salama na wananchi wawe salama na MALI zao
Hayo ameyasema ktk mkutano wa hadhara mjini Chunya alipokuwa akisikiliza Kero za wananchi na kuwaonya majambazi popote yalipo yasipange Mipango YA kufika ktk Mkoa huo
Amesema jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya nimefanya kazi kuwa YA kudhibiti ujambazi na hivi karibuni limekamata majambazi yalikuwa yakitafutwa kutoka Mikoa YA Tanga na Mbeya na hata yaliyojaribu kufanya uhalifu wilaya YA chunya yote yalinyanganywa silaha Haraka
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuyafichua majambazi
Aidha kwa taarifa alizonazo Wilaya YA Chunya ni wilaya inayomezewa mate na majambazi kutokana na shughuli za madini hivyo ni vema tukatoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi kudhibiti njama, mipango na matukio ya ujambazi
Amewahakikishia wananchi kuwa serikali YA mkoa chini YA uongozi wake hawatakubali majambazi kutamba na kufanya matukio bali wamejipanga kuona Mkoa unaendelea kuwa shwari na hao majambazi wautangaze Mkoa wa Mbeya kuwa si mkoa rafiki kwao na Amewataka polisi kuwa imara na akawasisitiza kwa kauli “WAKIJA NA MOTO NENDENI NA MOTO hakuna diplomasia ktk kupambana na Jambazi”
No comments