Trump apata uteuzi rasmi wa chama cha Republican kuwania urais
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump.
Bila ya kutarajiwa akiwa ameingia katika nafasi ya juu kwenye uwanja
wa siasa za Marekani, bilionea Donald Trump amepata rasmi uteuzi wa
chama cha Republican kuwania urais kwa mujibu wa hesabu ya wajumbe
iliyofanywa na shirika la habari la Associated Press-AP.
Akiwa amebakiwa na wagombea wachache kati ya 17 wa chama Republican waliokuwa wakiwania pamoja naye na hivyo kujiondoa mapema mwezi huu katika kinyang’anyiro AP imesema Trump ambaye aliwahi kuendesha kipindi cha televisheni hivi sasa anahakikishiwa kuwa ana wingi wa wajumbe 1,237 wanaohitaji katika mkutano mkuu wa Republican utakaofanyika mwezi Julai ambapo atateuliwa rasmi kuwania urais.

Donald Trump akiwa North dakota na wafuasi wake
Anatarajiwa huenda akapata mamia ya wajumbe katika uchaguzi wa
awali ambao utafanyika June 7. Nina heshima kubwa Trump aliwaambia
waandishi wa habari katika jimbo la kaskazini la North Dakota na kuapa
kwamba siku za kwanza za urais wake atatengua amri nyingi za kiutendaji
ambazo zilitiwa saini na Rais Barack Obama na kulijenga tena jeshi la
nchi.
No comments