Header Ads

JOSE MOURINHO KUSAINI MAN UNITED KABLA IJUMAA KWISHA!


Jose Mourinho anatarajiwa kusaini Mkataba wa kujiunga na Manchester United kabla Ijumaa kwisha licha ya kwamba mazungumzo ya pande hizo mbili yanaweza kwisha Leo.
Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes yupo kwenye mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Wooward, ambayo yamechukua muda kutokana na utata wa Umiliki wa Haki za Matangazo na Picha kwa upande wa Mourinho.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na Sky Sports, mazungumzo hayo yamepiga hatua na kupata muafaka kwenye ishu nyingi zilizokuwa zikikwamisha na zilizobaki zinatarajiwa kumalizika hii Leo.
Kila upande sasa unategemea Mkataba rasmi utasainiwa Ijumaa.
Hii Leo mambo ya jambo ambalo limemalizwa ni ile ishu ya Jina la Jose Mourinho mwenyewe kumilikiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea kwa kuuzia bidhaa zao kadhaa
Mwenyewe Mourinho inasemekana amehimiza mazungumzo hayo yaishe haraka huku yeye mwenyewe akiwa tayari ashaafiki kuhusu Mshahara na Maslahi yake binafsi ili aanze haraka kazi ya kuijenga upya Man United.

No comments

Powered by Blogger.