NEC wamerudisha fedha zilizobaki kwenye uchaguzi kwa Rais Magufuli na tayari zimepangiwa matumizi
June 07
2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia kwa mwenyekiti wa Tume Jaji
Mstaafu Damian Lubuva imekabidhi hundi ya Bilioni 12 kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, zilizobaki baada ya
uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika tarehe 25
Oktoba, 2015.
“tulijibanabana
sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa
sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo
wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri“ Jaji Mstaafu Lubuva.
Akizungumza
baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli
ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuokoa fedha hizo na
kuzirejesha serikalini ili zipangiwe majukumu mengine na ametaka taasisi
nyingine za serikali ziige mfano huo wa uzalendo na kutanguliza maslai
ya taifa.
“mlipewa zaidi ya Shilingi Bilioni
270, mkatumia shilingi Bilioni 261.6, mkabakiza shilingi Bilioni 12,
mngeweza kuamua kusema hamkubakiza na hakuna mtu yeyote ambaye
angewauliza, na saa nyingine pengine hakuna mtu yeyote ambaye angejua,
mngeweza pia kusema kiasi mlichotupa hakijatosha, tunaomba mtuongezee
ama mngetengeneze maneno mazuri mazuri ya matumizi, bado nina uhakika
serikalini wasingejua”
Rais Magufuli amelikubali ombi la tume kujengewa ofisi na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.
Rais
Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko
wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili
ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa
kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia
uchaguzi huo.
No comments