Mambo matano yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Zitto Kabwe na Polisi
Kupitia ukurasa wake wa facebook chama cha ACT Wazalendo kimeainisha masuala matano muhimu yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.
1.Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia”.
2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini”
3. Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni “Vilaza”
4. Kumgombanisha Rais na
Wananchi kwa Kusema “Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu
hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita “Vilaza”) na hivyo kumgombanisha na
wasio Masikini”
5. Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla
Kupitia ukurasa huo wametoa taarifa
kuwa maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye
Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani “Kutumia Maneno ya Matusi
yenye Kuweza Kuvunja Amani” (Abusive Language).
Jeshi la Polisi limemuomba Zitto afike
Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi. Mwanasheria
wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani
Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli
Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.
No comments