Mrema awajibu wapinzani wanaomsema Rais Magufuli hazingatii haki za binadamu, katiba
June 14
2016 Mwenyekiti wa chama cha TLP na mbunge wa zamani wa jimbo la vunjo
Agustino Mrema amekutana na vyombo vya habari nakuzungumza mambo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka vyama vya upinzani kutomhukumu Rais Magufuli kwa sababu hana nia ya kuua upinzani kama wanavyodai.
Mbele ya
waandishi wa habari Mrema amesema wapinzani ndio waliokubuhu katika
kuvunja haki za binadamu, sheria katiba na demokrasia, kama
walivyomfanyia na kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo
la Vunjo.
Hizi ni sentensi za mrema……>>>‘kwanza
ninachotaka kusema ni kwamba nataka kuonyesha wapinzani si wazuri
kama wanavyotaka Taifa liwaamini si wakweli na wananchi wawe macho sana
wasifikiri kila mpinzani ni mkweli wanayoyafanya ni haya lazima
tuyafichue lazima yasemwe waziwazi‘
>>>’kwahiyo
mimi ninachotaka kusema ni kwamba wala sisemi haya kwasababu ya kutaka
kufukua makaburi, nataka watu wajue kwamba wapinzani vitendo
wanavyovifanya sio vya haki wamtendee haki Rais, wampe nafasi aongoze nchi hii wasimsingizie vitu vingi’
>>>Mimi
ni mpinzani lakini nitaendelea kuwasema wapinzani ambao hawana
deomokrasia, hawazingatii haki za binadamu wala hawazingatii katiba,
sheria ni mafisadi mimi nitawasema, uwe CCM mimi nitakusema, uwe
upinzani nitakusema, wala siogopi wala sitaacha mimi sio CCM mimi ni
mpinzani , mzalendo na mkweli‘
No comments