Wanafunzi 7802 waliofukuzwa UDOM kuiburuza serikali mahakamani
Mmoja wa wakilishi wa wanafunzi hao akizungumza alisema kuwa wanafunzi waliofukuzwa walifaulu vizuri mitihani yao ya kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza, la pili na la tatu, hivyo kuwaita vizala ni kuwadhalilisha.
Aidha ameeleza kuwa walipofaulu waliomba kujiunga na programu hiyo maalumu na kwamba wangeweza kwenda kidato cha tano lakini waliamua kuja chuoni hapo.
Aidha ametaka serikali imelizane na walimu waliokuwa wanawafundisha ili waweze kurejea chuoni hapo kuendelea na masomo kwani hawapo tayari kwenda kuanza kidato cha tano kwani tayari wameshatumia muda mwingi chuoni.
Aidha amesema kuwa kama serikali haitakuwa tayari kutimiza malengo hayo, wao watachukua hatua zaidi na kwenda kutafuta haki yao mahakamani.
No comments