Makubaliano ya Rais Magufuli na Balozi wa Oman wakati akimuaga Ikulu jijini Dar es salaam
Rais
John Pombe Magufuli ameagana na Balozi wa Oman hapa nchini Saoud Ali
Mohamed al Ruqaishi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa
nchini.
Akizungumza
na Balozi huyo, Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameishukuru
Oman kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa kihistoria na kidugu na
Tanzania na ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano ipo tayari
kuongeza ushirikiano huo.
Tanzania
kwa kushirikiana na nchi za Oman na China zimekubaliana kutekeleza
mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani. Rais
Magufuli pia amemuomba Balozi Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi kufikisha
salamu zake kwa Sultani wa Oman Mtukufu Qaboos bin Said al Said………
>>>”Naomba
umfikishie salamu zangu za dhati Mtukufu Qaboos bin Said al Said,
Sultan wa Oman na umwambie tunamkaribisha Tanzania na nitafurahi kuona
mradi wa uwekezaji wa Bagamoyo unakuwa kielelezo cha undugu na urafiki
wetu uliodumu kwa miaka mingi”
No comments