Header Ads

Majibu ya dharau ya msaidizi wa Charles Kitwanga yafikishwa mbele ya uongozi wa Bungeni


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni ameingia matatani baada ya baadhi ya wabunge kumshitaka katika uongozi wa Bunge kuwa anatoa majibu ya dharau.
Katika gazeti la Nipashe Mbunge mmoja amenukuliwa akisema kuwa Naibu Waziri huyo amekuwa akijibu kwa dharau pindi anapoulizwa swali kitu ambacho kinawakera wabunge ambao huwa wanauliza maswali.
Imeripotiwa kuwa katika swali la nyongeza ambalo Mbunge Ally Keissy aliuliza, Naibu Waziri huyo alimjibu kuwa Wabunge wajenge nyumba za Polisi. Kitu hicho kilimkera mbunge huyo na kuamua kufikisha malalamiko yake kwa uongozi wa Bunge.
5Hili ni gazeti la Nipashe lililoripoti taarifa hiyo.

No comments

Powered by Blogger.