Utendaji wa Mkuu wa Wilaya Wakwaza Madiwani Morogoro
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamesa hawajaridhishwa na utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, John Henjewele kushughulikia migogoro ya ardhi inayoendelea wilayani humo.
Waliyasema
hayo katika mkutano na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya utatuzi wa migogoro ya
ardhi wilayani humo.
Diwani
wa Mbigiri, Juma Rajab alisema amejaribu kufika ofisini kwa mkuu huyo
wa wilaya kuhoji uhalali wa mashamba kuendelea kushikiliwa na wawekezaji
hewa ambao hawayaendelezi, lakini hapati ushirikiano.
Diwani
wa Kata ya Makole, Anfas Kaunda alimueleza Lukuvi kuwa kuna shamba
namba 35 lililopo Kijiji cha Mambeya ambalo lilifutiwa hati na
kurejeshwa serikalini tangu 1984, lakini hadi leo halijakabidhiwa kwa
kijiji.
Akizungumza
baada ya mkutano, Henjewele alisema diwani huyo ana mgogoro na wananchi
wake ambao amewakodisha mashamba ya Serikali kwa gharama kubwa.
No comments