JOHN KITIME NDIE KATIBU MKUU MPYA WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania leo amemtangaza John Kitime
kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo
ulifanyika mwezi wa pili na vyam 8 vya Shirikisho hilo kuchagua viongozi
wake. Nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa wazi. John Kitime ni mwanamuziki wa
bendi ya Kilimanjaro (Wananjenje), ambaye miaka ya 90 alikuwa
Mwenyekiti wa CHAMUDATA na wakati huo chama kilikuwa katika ufanisi
mkubwa wa kuweza hata kuwa na ushirikiano na mashirika ya miasaada ya
nje yaliyowezesha chama hicho kupata misaada mbalimbali, na hata kufanya
matamasha makubwa ya muziki. Pia Kitime ni Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wanamuziki chama ambacho pia kimewezesha wanacham wake kupata bima ya
Afya. Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mkuu huyo alisema
kati ya mambo atakayoanza nayo ni kuimarisha Shirikisho kwa kuimarisha
vyama wanachama wa Shirikisho, ikiwemo kuhamasisha kuanzishwa vyama
vingine. Kuonyesha kuwa anania ya kutekeleza hizo mwisho wa mkutano huo
aliwahamasisha waandishi wa habari za muziki kuanzisha chama chao. Vyama
vilivyo wanachama wa Shirikisho la Muziki Tanzania ni Chama cha Muziki
wa Dansi Tanzania CHAMUDATA, Chama cha Muziki wa Rumba CHAMURUMBA, Chama
Cha Muziki wa Injili Tanzania CHAMUITA, Tanzania Folk Music Development
Association TAFOMUDEA, Tanzania taarab Association TTA, Tanzania Urban
Music Association TUMA
No comments