Baada ya vyama vya siasa kuonesha nia ya mikutano, maandamano, Jeshi la polisi limekuja na hii taarifa
June o7
2016 Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa inayosema kwamba wamepokea
taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano
na maandamano hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya
mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la
kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).
Aidha
vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho
kitasemwa na wapinzani wao. Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba
upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya
kisiasa.
kupitia
taarifa hiyo Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano na
mikutano ya hadhara kuanzia June 07 2016 hadi hapo hali ya usalama
itakapotengemaa.
Jeshi la
Polisi limewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi
kutotii sheria za nchi. Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua
kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi
agizo hili.
Aidha
taarifa hiyo imewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la
kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee
kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
No comments