Mikataba ya Polisi Yaitishwa Wizarani
BAADA
ya Rais John Magufuli kuizungumzia mikataba ya ujenzi ya Jeshi la
Polisi iliyoingia na wawekezaji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi ameitisha mikataba yote ya jeshi hilo.
Jeshi
la Polisi nchini limetakiwa kuwasilisha mikataba ya miradi ya ujenzi wa
nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha
Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ule wa majengo
mbalimbali ya mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia mkataba naye.
Agizo
hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira ikiwa ni miezi miwili tu tangu Rais
Magufuli kuzungumzia mikataba hiyo na kuitilia shaka wakati akifungua
kikao kazi cha makamanda wa Polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa
serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi mjini Dodoma.
Meja
Jenerali Rwegasira alisema mradi huo ni mkubwa na wa muda mrefu na
hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha mkataba huo, ambao utekelezaji
wake unaendelea ili aufahamu vizuri mkataba huo, unaolihusisha Jeshi la
Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania Limited.
Kwa
mujibu wa taarifa ya wizara hiyo jana kwa vyombo vya habari, Katibu
Mkuu huyo ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo
katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni, ambako zinajengwa nyumba za
kuishi askari wa Jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
Mradi
mwingine alioutembelea ni ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi
Oysterbay na kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua
iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya Jeshi la Polisi.
Katika
mradi huo wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Oysterbay, unaotekelezwa na
mwekezaji Kampuni ya Mara World Tanzania Limited, pia kutajengwa ofisi
za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.
Rais
Magufuli wakati akihutubia makamanda hao wa Polisi Aprili mwaka huu,
alisema miongoni mwa vitu ambavyo vinalisumbua jeshi hilo ni mikataba ya
hovyo akisisitiza umuhimu wa fedha za jeshi hilo kutumika vizuri.
Rais
Magufuli alisema kuna taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi, limekuwa
likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha, hali inayoongeza ukubwa wa
matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Alitoa
mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha, zinazotolewa kwa ajili ya
kununua vifaa na sare za askari ama mikataba yenye mashaka inayotiwa
saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza
hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
“Oysterbay
pale ni eneo ambalo ni zuri sana, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye
mikataba mnayoijua ninyi, mkapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama
majengo hayo yanafaa.
“Palikuwa
na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati
kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka
kitega uchumi na polisi wenu wakakaa pale?
No comments