Wabunge wengine wanne wa CHADEMA hatihati kutimuliwa kuhudhuria vikao vya Bunge
Kila siku
asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti
ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya
Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya story kubwa June 06 2016 kwenye gazeti la Raia Tanzania ni hii yenye kichwa cha habari ‘Wabunge wengine kutimuliwa’
Gazeti la
Raia Tnzania limeripoti kuwa wabunge wanne wote kutoka CHADEMA wako
hatihati ya kutimuliwa kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti
linaloendelea mjini Dodoma kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali
za bunge, huku Mbunge wa Bunda mjini Esther Bulaya, akitarajiwa
kuongezewa adhabu kubwa zaidi ya anayoitumikia kwa sasa.
Gazeti
hilo limesema kuwa habari za kuaminika kutoka ndani ya kamati ya
maadili, haki na madaraka ya bunge zimewatajwa wabunge hao wa CHADEMA
kuwa ni Mbunge wa Simanjiro, James Millya, Mbunge wa Viti maalum, Suzan Lymo, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Gazeti hlo
limeripoti kuwa wabunge hao kwa pamoja kwa nyakati tofauti, wanadiwa
kufanya makosa tofauti ya kikanuni katika mkutano wa bunge la bajeti
linaloendelea Dododma, yakiwemo ya kuhamasisha vurugu ndani ya ukumbi wa
bunge
No comments