Mbunge asema Tanzania na Sudani Kusini zinafadhili upinzani kuandamana nchini Kenya
Mbunge
wa Starehe, Maina Kamanda nchini Kenya Mei 30 alisema kuwa Tanzania na
Sudan Kusini ni miongoni mwa nchi zinazofadhili upinzani kusababisha
machafuko nchini Kenya.
Msemaji
wa serikali Eric Kiraithe alitoa madai sawa na mbunge huyo lakini
hakutaja majina yoyote. Alisema kuwa wanofadhili upinzani nchini Kenya
wangtajwa mara baada uchunguzi ni kamili.
Hii
inakuja wakati CORD na washirika wamekuwa wamekuwa wakifanya maandamano
kila wiki kupambana wakitaka Tume ya Uchaguzi (IEBC) iundwe upya kabla
ya uchaguzi.
“Raila
amekuwa akizunguka nchi nzima. Tunajua kuwa anafadhiliwa na serikali
hizi mbili kwa lengo la kuiyumbisha Kenya. Wewe endelea tu lakini sisi
hatutakuruhusu” alikaririwa Maina Kamanda akizungumza.
Maina
Kamanda aliyasema hayo siku hiyo hiyo ambapo msemaji wa Serikali Eric
Kiraithe alitoa tuhuma hizo hizo. Katika tamko lake alisema kuwa nchi
mbili majirani na Kenya zinafadhili upinzani kuiyumbisha Kenya.
“Uchunguzi
uliofanyika umedhihirisha kuwa kuna watu ndani ya serikali
wanashirikiana na nchi mbili za jirani na Kenya kuleta hali ya
machafuko, uvunjifu wa amani na sheria” alisema Eric Kiraithe
Hakumtaja mtu yeyote lakini alidai kuwa uchunguzi ukikamilika atawataja watu hao na nchi wanaoshirikiana nazo.
Kiongozi
CORD Raila Odinga ni rafiki wa karibu wa Rais wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli. Raila Odinga mapema mwezi wa nne alimtembelea Rais
Magufuli alipokuwa mapumzikoni nyumbani kwa Chato.
Uhusiano
wa Raila na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir haufahamiki sana japo
anaukaribu mkubwa na makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan John Garang.
Garang alishika wadhifa huo tangu Julai 9, 2005 hadi Julai 30, 2005.
Alifariki katika ajali ya Helcopter alipokuwa akitokea kwenye mkutano na
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
No comments