Header Ads

Juni 16 kila mwaka ni siku ya Mtoto Wa Afrika, fahamu zaidi kuhusu siku hii


Leo Juni 16, 2016 ni maadhimisho ya siku ya Mtoto wa  Afrika ambapo shughli na majadala mbalimbali hufanyika ikiwa na lengo la kulinda na kumuinua mtoto wa Afrika.
HOPE3
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Africa.
wccelc-group-shot
Mwaka kuu maadhimisho hayo yanafanyika yakiwa na kaulimbiu kubwa ya kuwalinda watoto wetu dhidi ya ukatili (ubakaji, ulawiti) ambao watoto wamekuwa wakifanyiwa katika jamii na hivyo kukwamisha maendeleo yao.
1-
Akizungumzia suala la udhalilishaji wa watoto katika jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  amesema yupo tayari kuleta mabadiliko ya sheria ambapo pindi mwanaume atakapothibitika kuwa amembaka au kumlawiti mtoto basi ahasiwe.

No comments

Powered by Blogger.