Header Ads

Linah asema amefurahi kuona Ex wake anafunga ndoa na mwanamke mwingine

Msanii wa muziki, Linah Sanga amesema anampongeza Ex wake kwa kufunga ndoa na mwanamke mwingine kwani anaamini hiyo haikuwa bahati yake.


Akiongeza na Bongo5 Alhamisi hii, Linah amesema licha ya kuachana na Ex wake huyo miezi kadhaa iliyopita, lakini bado alikuwa anawasiliana naye na taarifa za kufunga ndoa alikuwa yazo.
“Katika hali ya kawaida nimejisikia poa kwa sababu nilishaacha naye, kwa hiyo mimi nilikuwa namtakia mazuri siku zote, na ndo maana tulikuwa washikaji,” alisema Linah.
Pia Linah amesema wakati Ex wake anafanya mipango ya kuoa alikuwa anawasilianaye pamoja na kupewa taarifa mbalimbali ya vitu vinavyoendelea.
Pia muimbaji huyo wa wimbo ‘Ole Themba’, amesema alishindwa kuhudhuria ndoa ya Ex wake kutokana na kuwa busy na kazi.

No comments

Powered by Blogger.