Kesi ya Messi: Mwendesha Mashtaka na Mwanasheria mkuu wametoa ushauri huu kwa hakimu
Katika taarifa yake rasmi aliyoitoa leo hii, mwendesha mashtaka huyo amesema kwamba hakukuwa na jaribio lolote la Messi kukwepa kodi na hivyo amemshauri hakimu kumuachia huru nahodha huyo wa Argentina. Hata hivyo, mashtaka dhidi ya baba ya mchezaji huyo, Jorge Messi, yataendelea kusimama na mwendesha mashtaka ameshauri aadhibiwe kwenda jela kwa miezi 18.
Kwa upande wa mwanasheria wa serikali wmeendelea kusisitiza kwamba Lionel Messi alikuwa anafahamu kuhusu makampuni yaliyotengenezwa katika kukwepa kodi. Wanataka Messi na baba yake wapigwe nyundo ya miezi 22 kila mmoja.
Baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi, Messi amesafiri kuelekea Marekani kuungana na timu yake ya taifa kwa ajili ya michuano ya Copa America.
No comments