VIDEO: Hatua ya serikali baada ya kupiga STOP uvunaji misitu Chunya,Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbeya Rehema Madusa
amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mpango wa serikali
baada ya kutoa zuio la ukataji miti inayotumika katika shughuli za
kibiashara ikiwemo uchomaji mkaa katika wilaya yake huku akiagiza
kusimamishwa kazi kwa afisa wa TFS kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa misitu.
DC Rehema amesema…>>>’Kutokana
na uvunaji holela wa mazao ya misitu katika Wilaya ya Chunya pamoja na
uvujaji wa mapato ya mazao ya misitu nasitisha zoezi la uvunaji wa mkaa,
mbao na magogo katika wilaya yetu ya Chunya kuanzia November 1 2016‘
‘Mamlaka za misitu itatakiwa
kutotoa leseni za mazao tajwa kuanzia October 1 2016 pia itatakiwa
kuwakamata wavunaji wote wasio na vibali‘ –DC Rehema Madusa
‘Mwisho
wa kusafirisha mazao yote yaliyohakikiwa ni October 30 2016, na yeyote
atakayepatikana baada ya tarehe tajwa akisafirisha mazao hayo
atashughulikiwa kisheria na mamlaka husika‘ –DC Rehema Madusa
‘Ninamwagiza mkurugenzi mkuu
wa TFS kumsimamisha ofisa wa TFS wakati tunajipanga kuchukua hatua za
kisheria baada ya kubainika na tuhuma za kuwasaidia wavunaji wasio na
vibali halali kusafirisha mazao ya misitu‘ –DC Rehema Madusa
Unaweza kuendelea kumsikiliza DC Rehema kwenye hii video hapa chini…
No comments